- (+255) 24-2230271
- info@zstcznz.org
- Mon - Fri: 07:30 - 15:30
Kamati ya Kilimo na Biashara ya Baraza la Wawakilishi yaridhishwa na Utendaji wa ZSTC
Kamati ya Utalii, kilimo na Biashara ya Baraza la Wawakilishi imelipongeza Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) kwa juhudi walizochukua za kuyarudisha baadhi ya maeneo yalioharibiwa kutokana na shughuli za uchimbaji wa mchanga Zilizopelekea eneo hilo kuathirika na athari za kimazingira.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe,Mtumwa Pea Yussuf katika ziara ya kutembelea na kukagua Mashamba na Viwanda vya Shirika hilo Pemba ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukum ya Kamati hiyo.
Aidha amesema ipo haja Kwa Shirika kushirikiana na jamii katika kutunza Rasilimali zilizopo za Ofisi ili ziweze kuleta tija kwa jamii kwa kuongeza uzalishaji hasa kupitia viwanda vya uzalishaji wa mafuta ya Mimea.
Akizungumza katika Ziara hiyo Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC)Nd. Soud Saidi Ali amesema kuwa, Shirika litaendelea kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyo tolewa na Kamati hiyo ili kuleta mabadiliko ndani ya Shiraka.
Katika hatiua nyengine Mkurugenzi Soud amewataka Wafanyakazi wa Shirika hilo kushirikiana na kua na umoja katika kazi ili waweze kuleta maendeleo na kufikia malengo yaliyokusudiwa ndani ya Shirika.
Kwa upandewake Bwana Shamba kutoka Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Nd. Haji Mussa Haji ameeleza kuwa Shirika litatoa Mashirikiano kwa jamii katika namna bora ya utumiaji wamashamba hayo iliywawezekutumika kama yalivyokusudiwa na Serikali. hivyo kupitia Shirika la ZSTC wataendelea kutoa elimu kwa jamii kila inapohitajika alisema.
Ziara hio ya siku moja ya kamati ya Utalii Kilimo na Biashara ya Baraza la Wawakilishi imetembelea Sehemu mbalimbali ikiwemo mashamba ya Mikaratusi ya kutengenezea mafuta yaliopo kishindeni Mkoa wa Kaskazini Pemba,Shamba la mamoja, na kutembelea na kukagua vyungu vya kukamulia Mafuta vilivyopo mtakata chake chake Pemba.
The best quality of cloves in the market that has a strong taste and aroma.